Vita ya Diego Costa na Chelsea
imepamba moto baada ya mshambuliaji huyo kukataa ombi la kurejea
London na kusisitiza hana mpango wa kuondoka nchini Brazili na kwa
sasa anajifua kwenye gym.
Costa kwa sasa anaishi nyumbani kwao
katika mji wa Lagarto baada ya meneja Antonio Conte kumtumia ujumbe
wa maandishi uliomueleza hayupo tena katika mipango yake ya Chelsea.
Costa pia amedai kuwa Chelsea
inataka kumlazimisha kufanya mazoezi na kikosi cha akiba iwapo
atarejea. Tayari amepigwa faini ya laki 3 na huenda akapigwa faini
nyingine akiendelea kugoma kurejea.
Diego Costa akiwa kwenye gym nchini Brazili baada ya kugoma kurejea Chelsea
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni