Kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga amesema atafungua
kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais wa wiki iliyopita ambao
anadai uligubikwa na udanganyifu.
Bw. Odinga, ambaye alishindwa na rais aliyepo madarakani Uhuru
Kenyatta, ameituhumu mamalaka ya uchaguzi kwa udanganyifu uliopelekea kuiua
demokrasia.
Hata hivyo waangalizi wa kimataifa waliuelezea uchaguzi huo
ulikuwa ni huru na wa haki. Jumuiya ya kimataifa inahofia tuhuma za wizi wa
kura zinaweza kuibua machafuko.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni