Serikali ya Zimbabwe imetaka kupatiwa kinga ya Kidiplomasi
mke wa rais Robert Mugabe, Grace dhidi ya kesi ya shambulizi la kudhuru mwili
dhidi ya mwanamke mmoja raia wa Afrika Kusini.
Grace Mugabe bado yupo Afrika Kusini kwa mujibu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani, ikiwa ni kinyume na taarifa za awali ambazo zilisema kuwa amesharejea
Zimbabwe.
Mwanamitindo raia wa Afrika Kusini mwenye miaka 20,
amemtuhumu Garce Mugabe kwa kumjeruhi katika hoteli moja Jijini Johannesburg siku
ya jumapili.
Polisi nchini Afrika Kusini walitarajia Grace Mugabe kujisalimisha
jana ili kufikishwa Mahakamani lakini hakufanya hivyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni