Kiungo wa timu ya PSG Blaise Matuidi amepiga picha akipozi
na skafu ya Juventus akiwa uwanja wa ndege wa Turin kukamilisha uhamisho wake
wa paundi milioni 18.
Matuidi amewasili Juventus ambapo mchezaji huyo Mfaransa atafanyiwa
vipimo vya afya yake baada ya kukubali mkataba wa miaka mitatu.
Matuidi anakuwa mchezaji wa 10 kuwasili katika klabu ya ligi
ya Seria A katika kipindi hiki cha uhamisho wa majira ya joto.
Mfaransa Blaise Matuidi akionyesha ishara ya vidole gumba akiwa uwanja wa ndege kuashiria mambo safi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni