.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 16 Agosti 2017

WAZIRI MWAKYEMBE AHIMIZA MASHIRIKIANO KATI YA WIZARA NA UNESCO KATIKA KUHIFADHI HISTORIA YA NCHI

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania Bibi. Zulmira Rodrigues wakati wa kikao na watendaji wa Wizara pamoja na UNESCO kujadili mashirikiano yaliyopo katika kuhifadhi historia ya nchi leo Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania Bibi. Zulmira Rodrigues (wapili kushoto) akizungumza wakati wa kikao na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja na watendaji wa Wizara kujadili mashirikiano yaliyopo katika kuhifadhi historia ya nchi leo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Msaidizi Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Benard Lubogo (katikati) akichangia mada wakati wa kikao na watendaji kutoka UNESCO kujadili mashirikiano yaliyopo katika kuhifadhi historia ya nchi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bibi. Martha Swai
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akipokea moja ya kitabu chenye kumbukumbu ya historia ya Afrika ikiwemo Tanzania kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania Bibi. Zulmira Rodrigues wakati wa kikao na watendaji wa Wizara pamoja na UNESCO kujadili mashirikiano yaliyopo katika kuhifadhi historia ya nchi leo Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara yake na watendaji kutoka UNESCO baada ya kikao na watendaji hao kujadili mashirikiano yaliyopo katika kuhifadhi historia ya nchi leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa UNESCO nchini Tanzania Bibi. Zulmira Rodrigues na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bibi. Martha Swai

                                                       Picha na: Genofeva Matemu -WHUSM

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni