Timu ya Manchester United imefunga
magoli matatu ndani ya dakika nne na kuendeleza wimbi la ushindi kwa
kuibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Swansea.
Katika mchezo huo Eric Bailly,
Romelu Lukaku, Paul Pogba na Anthony Martial walifanikisha kupatikana
kwa ushindi huo wa kikosi cha Jose Mourinho.
Jordan Ayew alikuwa wa kwanza kukosa
kosa goli kwa kupiga shuti lililogonga mwamba, kabla ya baadaye Eric
Bailly kuipatia Manchester United goli la kuongoza.
Romelu Lukaku aliongeza goli la pili
kwa Manchester United katika dakika ya 80 kwa shuti la karibu kisha
Pogba akafunga la tatu kambla ya Anthony Martial kufunga la nne.
Beki Eric Bailly akiuwahi mpira wa kichwa uliopigwa na Paul Pogba uliogonga mwamba na kuuzamisha kimiyani
Paul Pogba akifunga kiufundi goli la tatu la Manchester United
Anthony Martial akiachia shuti na kufunga goli la nne la Manchester United
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni