Sadio Mane ameipatia Liverpool
ushindi wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa kuifungia goli
moja na kuifanya Crystal Palace ikubali kipigo cha pili katika msimu
huu.
Kikosi cha Jurgen Klopp kilikuwa
kama kinaelekea kutoka sare kufuatia kandanda zuri waliotandaza
Crystal Palace lakini Mane aliweza kumpoteza kipa Wayne Hennessey.
Crystal Palace, ilifungwa magoli 3-0
nyumbani katika mchezo wa kwanza dhidi ya Huddersfield ilikosa
nafasi ya kufunga kabla ya Mane kutikisa nyavu.
Sadio Mane akifunga goli pekee katika mchezo huo likiwa ni goli lake la pili katika msimu huu
Sadio Mane akishangilia goli kwa kumrukia kocha wake Jurgen Klopp
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni