Zlatan Ibrahimovic inaonekana
ameanza kupona jeraha lake la goti alilopata baada ya kuonekana
akiruka kutoka juu ya boti ya kifahari na kutumbukia majini akiwa
Riviera Ufaransa.
Mchezaji huyo raia wa Sweden amekuwa
akiharakisha kupona kwake akipitia kipindi cha kuimarisha zaidi mguu
ulioumia, na ametumia kipindi hiki kuwa na familia yake huko Cannes.
Zlatan Ibrahimovic akiwa ameruka juu huku familia yake ikimuangalia
Zlatan Ibrahimovic akiwa amechupa kuelekea majini katika kujiweka fiti
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni