Andre Silva amefunga magoli matatu
yaani hat-trick wakati AC Milan ikianza kwa kishindo mechi yao ya
kwanza ya Ligi ya Uropa kwa kuichakaza Austria Vienna magoli 5-1.
Silva alisajiliwa kutoka Porto kwa
dau la paundi milioni 34 na Milan, ambayo inashirikia Ligi ya Uropa
kwa mara ya kwanza tangu miaka minne kupita.
Klabu hiyo ya Italia imetumia kitita
cha paundi milioni 170 katika usajili uliomalizika, ikiwemu mchezaji
mpya Calhanoglu aliyefunga goli la kwanza na Suso kufunga la tano.
Mfungaji wa magoli matatu hat-trick, Andre Silva akifunga moja ya magoli yake
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni