Kocha Arsene Wenger alishangazwa
mchezo wa Ligi ya Uropa wa Arsenal kuendelea kufanyika kwa ghasia za
mashabiki wasio na tiketi katika mchezo dhidi ya Cologne.
Mashabiki wa wageni Cologne wapatao
20,000 walijitokeza London, licha ya klabu hiyo ya Ujerumani
kutengewa tiketi 2,900.
Baada ya Arsenal kushinda kwa magoli
3-1 jana katika dimba la Emirates Stadium, Kocha Wenger amesema
tunaishi katika jamii inayohitaji ulinzi kwa asilimia 100.
Askari wa Jiji la London wakiwazuia maelfu ya mashabiki wa Cologne wasio na tiketi
Askari pia walilazimika kutumia mbwa katika kutuliza ghasi za mashabi wa Ujerumani ndani ya uwanja wa Emirates
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni