Timu ya Chelsea imeibuka na ushindi
mnono wa magoli 6-0 dhidi ya timu ya Qarabang katika mchezo wa Ligi
ya Mabingwa Ulaya huku Michy Batshuayi akitupia wavuni magoli mawili
na Davide Zappacosta akifunga goli
zuri.
Chelsea imerejea kwa kishindo katika
ligi hiyo baada ya kushindwa kufuzu msimu uliopita, katika mchezo
huo iliwapumzisha wachezaji wake kadhaa wa kikosi cha kwanza dhidi ya
timu ngeni ya Azerbaijani, lakini ikashinda.
Katika mchezo huo magoli la Chelsea
yalifunga na Pedro dakika ya 5, Zappacosta dakika ya 30, Azpilicueta
dakika 55, Bakayoko dakika 71, Batshuayi magoli mawili, Medvedev naye
akajifunga dakika ya 82.
Pedro akifunga kiufundi goli la kwanza la Chelsea katika mchezo huo
Cesar Azpilicueta akifunga goli la tatu la Chelsea katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni