John Stones amefunga mara mbili
wakati Manchester City ikianza kampeni ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa
ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya timu ya Feyenoord huko Rotterdam.
Katika mchezo huo Stones aliifungia
Manchester City goli lao la mapema zaidi katika michuano hiyo kwa
mpira wa kichwa baada ya dakika mbili tu.
Sergio Aguero aliongeza goli la pili baada ya dakika 10, Gabriel Jesus akaongeza la tatu kisha John Stones
akakamilisha karamu kwa kufunga goli la nne.
John Stones akiwa juu baada ya kuupiga mpira kwa kichwa uliozaa goli la kwanza
Sergio Aguero akiifungia Manchester City goli la pili
Katika mchezo mwingine wa Ligi ya
Mabingwa Ulaya Liverpool ikicheza mchezo wao wa kwanza wa ligi hiyo
tangu mwaka 2014 ilitoka sare ya magoli 2-2 dhidi ya Sevilla ikiwa
Anfield.
Mohamed Salah akiifungia Liverpool goli la kusawazisha la pili
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni