Nigeria imefanikiwa kukata tiketi ya
kufuzu michuano ya fainali ya kombe la dunia baada ya kupata ushindi
dhidi ya Zambia.
Nigeria iliuanza mchezo huo ikijua
kuwa ushindi utawafanya wakate tiketi ya michuano hiyo na alikuwa
Alex Iwobi, aliyetokea benchi aliyewapatia ushindi.
Goli hilo lililofungwa na mchezaji
huyo wa Arsenal katika dakika ya 73, baada ya mchezaji wa Chelsea
Victor Moses na Abdullahi Shehu lkugongeana vyema.
Kocha wa Nigeria Gernot Rohr akirushwa juu kusherehekea ushindi



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni