.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 8 Oktoba 2017

CRISTIANO RONALDO ATOKEA BENCHI NA KUISAIDIA URENO KUSHINDA

Cristiano Ronaldo ametokea benchi na kuisaidia Ureno kuifunga Andorra magoli 2-0 na kuhuisha ndoto yao ya kutinga fainali za kombe la dunia.

Nyota huyo wa Real Madrid alifunga goli katika dakika ya 63 kabla baadaye Andre Silva kukamilisha ushindi kwa kuongeza la pili.

Kwa ushindi huo Ureno ipo nyuma kwa tofauti ya pointi tatu na vinara wa kundi lao B, timu ya Switzerland, iliyoifunga Hungary magoli 5-2 huko Basel.

Ureno inahitaji kushinda mchezo wao wa mwisho katika kundi hilo dhidi ya vinara Switzerland siku ya jumanne ili iongoze kundi hilo.
     Mshambuliaji nyota Cristiano Ronaldo akiifungia Ureno goli katika mchezo huo
   Andre Silva akishangilia baada ya kutumbukiza mpira wavuni na kuiandikia Ureno goli la pili

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni