.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 8 Oktoba 2017

BLAISE MATUIDI AING'ARISHA UFARANSA IKIONGOZA KUNDI A

Shambulizi la Blaise Matuidi katika dakika ya tatu limetosha kuipatia Ufaransa pointi tatu na kuongoza kundi A, huku ukiwa umebakia mchezo mmoja wa kuwania kutinga fainali za kombe la dunia.

Kikosi cha Ufaransa kinachonolewa na Didier Deschamps, kilipata goli hilo lililofungwa na Matuidi baada kugongeana vyema baina ya wachezaji Lucas Digne na Antoine Griezmann na kuizamisha Bulgaria.

Wakati Sweden wakisafiri kwenda Uholanzi katika mchezo wao wa mwisho wakiwa pointi moja nyuma, Ufaransa sasa inaweza kukata tiketi ya kutinga fainali za kombe la dunia jumanne iwapo itaifunga Belarus. 
             Mfaransa Blaise Matuidi akijipinda na kufunga goli pekee katika mchezo huo
   Kiungo wa Chelsea N'Golo Kante akishikilia misuli ya paja wakati akitoka nje baada ya kuumia

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni