Kocha Ronald Koeman amesema
ataibadilisha Everton na kuweza kufanya vizuri baada ya kuporomoka
mkiani kufuatia kipigo cha magoli 5-2 dhidi ya Arsenal katika dimba
la Goodison Park.
Everton walijikuta wakiaibika kwa
kipigo hicho mbele ya mashabiki wao, ambapo hadi sasa hawajapata
ushindi katika michezo mitano katika michuano yote.Wayne Rooney
alifunga goli la kwanza kama alilowafunga Arsenal mwaka 2002.
Nacho Monreal aliisawazishia Arsenal
goli, kabla ya baadaye Mesut Ozil akaongeza goli la pili Alexandre
Lacazette akatumbukiza la tatu na Aaron Ramsey, Oumar Niasse
akaifungia Everton kabla ya Alexis Sanchez kufunga goli la tano.
Wayne Rooney akipiga mpira wa shuti la kuzungusha na kukumbushia alivyoitungua Arsenal mwaka 2002
Oumar Niasse akiifungia Everton goli la pili katika mchezo huo ulioishia kwa kufungwa magoli 5-2 na Arsenal
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni