Magoli mawili ya Harry Kane
yameichochea Tottenham kuiadhibu Liverpool yenye beki uchochoro
katika dimba la Wembley kwa kuichapa magoli 4-1 na kufikisha pointi
sawa na Manchester United katika nafasi ya pili.
Kane alifunga goli la kwanza baada
ya dakika nne tu baada ya pasi ya kubetua ya Kieran Trippier kupita
juu ya kichwa cha Dejan Lovren, na kumkuta mshambuliaji huyo wa
Uingereza aliyetumbukiza mpira kimiani.
Dakika nane baadaye Spurs wakaongeza
kupitia kwa Son Heung-min, lakini baadaye Liverpool wakachomoa goli
moja kupitia kwa Mohamed Salah. Dele Alli aliongeza goli la tatu na
kisha baadaye Kane akafunga goli la nne.
Harry Kane akifunga goli la kwanza la Spurs kati ya mawili aliyoyafunga
Dele Alli akiifungia Tottenham Spurs goli la tatu katika mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni