Edinson Cavani amefunga goli kali la
mpira wa adhabu katika dakika ya 93 na kuiokoa Paris St-Germain
kuambulia sare ya magoli 2-2 dhidi ya Marseille baada ya Neymar
kutolewa nje.
Luiz Gustavo alifunga goli la kwanza
la Marseille kwa shuti la umbali wa yadi 30, kabla ya Neymar
kusawazisha likiwa ni goli lake la kumi tangu atue PSG.
Florian Thauvin aliifanya Marseille
iongoze tena zikiwa zimebakia dakika 10 kabla ya Neymar kupewa kadi
za njano mara mbili ndani ya dakika mbili.
Mbrazil Neymar akiwa haamini baada ya kulambwa kadi nyekundu
Mpira uliopigwa na Edinson Cavani ukijaa wavuni na kuiokoa PSG kutoka sare
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni