Timu ya Real Madrid imerejea katika
nafasi ya tatu ya msimamo wa La Liga, baada ya kupata ushindi wa
kiulaini wa magoli 3-0 dhidi ya timu ya Eibar iyoyosuasua.
Mabingwa hao watetezi waliongoza kwa
magoli 2-0 hadi kipindi cha pili, yaliyopachikwa na Paulo Oliveira
aliyejifunga na kisha Isco kutumbukiza la pili.
Cristiano Ronaldo hakufanikiwa
kutikisa nyavu, lakini alikuwa beki Marcelo aliyetikisa nyavu na
kufunga goli la tatu baada ya kugongeana vyema na Karim Benzema.
Mchezaji wa Eibar Paulo Oliveira akijifunga wakati akijaribu kuokoa mpira
Beki wa Eibar, Arbilla akimkata
kwanja beki wa Real Madrid Mfaransa Theo Hernandez
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni