Matokeo ya awali ya urais Liberia
yanaonyesha kuwa mchezaji wa zamani wa soka George Weah anaongoza
mapema.
Takwimu za Tume za Taifa ya Uchaguzi
(NEC) zinaonyesha Weah anaongoza katika kaunti 11 zilizohesabiwa kura
kati ya kaunti 15.
Mpinzani wake mkuu, makamu wa rais
aliyemadarakani Joseph Boakai, yupo katika nafasi ya pili. Mshindi
anatakiwa kupata asilimia 50 za kura zote.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni