Waendesha mashtaka wa Uswizi
wamefungua uchunguzi wa makosa ya uhalifu dhidi ta Mwenyekiti wa timu
ya Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi.
Uchunguzi huo unahusiana na
uchunguzi unaoendelea kuhusiana na aliyekuwa Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) Jerome Valcke.
Makosa yanayochunguzwa yanahusika na
mauzo ya haki za kombe la dunia kwa Bein Sports, ambayo Al-Khelaifi
ni Mtendaji Mkuu wake.
Mwenyekiti wa PSG Al-Khelaifi akiwa na mchezaji Kylian Mbappe
Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) Jerome Valcke
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni