Kocha wa muda wa timu ya Everton
David Unsworth amesema timu yake imemfanya ajivune licha ya kupoteza
mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Chelsea.
Katika mchezo huo ulioishia kwa
magoli 2-1 Willian alifunga goli la pili na kuipeleka nusu fainali
Chelsea ya kombe la Carabao.
Chelsea ilipata goli lake la kwanza
kupitia kwa Antonio Rudiger kwa mpira wa kichwa huku goli pekee la
Everton likifungwa na Dominic Calvert-Lewin.
Rudiger akiwa ameruka juu kuupiga mpira kichwa uliozaa goli la kwanza la Chelsea
Mbrazil Willian akiwa ameachia shuti lililojaa wavuni na kuandika goli la pili
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni