Kocha wa West Ham Slaven Bilic
amesema kikosi chake kimeonyesha makali baada ya kutoka nyuma
kufungwa magoli mawili na kuibuka na ushindi dhidi ya Tottenham
katika kombe la Carabao.
Bilic amekuwa katika presha kwenye
Ligi Kuu ya Uingereza, alijikuta katika wakati mgumu tena jana
katika kipindi cha kwanza kwa kufungwa magoli 2-0 kabla ya mambo
kugeuka kipindi cha pili.
Mshambuliaji Andre Ayew alifunga
mara mbili kwa mashuti ya karibu na lango na kisha Angelo Ogbonna
akaifungia West Ham goli la tatu.
Mfaransa Moussa Sissoko akiifungia Tottenham goli la kwanza
Mshambuliaji Andre Ayew akishangilia baada ya kufunga goli
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni