Baada ya kutoka sare tasa na
Manchester United katika Ligi Kuu ya Uingereza safu ya ushambuliaji
ya Liverpool imezinduka katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuifunga NK
Marbori kwa magoli 7-0.
Katika mchezo huo Roberto Fermino na
Mohamed Salah wote walifunga magoli mawili wakati Liverpool ikipata
ushindi mkubwa wa ugenini, huku wakiutawala vilivyo mchezo huo wa
kundi E.
Magoli mengine ya Liverpool
yalifungwa na Philippe Coutinho, Alex Oxlade-Chamberlain pamoja na
Trent Alexander-Arnold ambaye alifunga goli la saba katika dakika ya
90 ya mchezo huo.
Roberto Fermino akiangali mpira wa kichwa alioupiga ukimshinda kipa na kujaa wavuni
Mohamed Salah akifunga goli huku Roberto Fermino naye akiwa amejipanga kuuwania mpira huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni