Kocha wa Manchester City, Pep
Guardiola, anahisi ushindi wa magoli 2-1 wa Ligi ya Mabingwa Ulaya
dhidi ya Napoli ulikuwa umetokana kiwango bora cha timu yake dhidi ya
timu bora aliyowahi kukutana nayo.
Katika mchezo huo ulioshuhudia safu
mbili hatari katika ushambuliaji Ulaya zikichuana, walikuwa ni Raheem
Sterling na Gabriel Jesus waliochangia kuipatia Manchester City
kupata ushindi kwa kufunga magoli hayo mawili.
Napoli inayoongoza ligi ya Serie A
kwa kushinda michezo yote nane katika msimu huu, walipatiwa penati
mbili katika mchezo huo moja iliyopigwa na Dries Mertens ikiokolewa
na nyingine ikifungwa na Amadou Diawara.
Raheem
Sterling akifunga goli la kwanza la Manchester City katika mchezo huo
Mbrazil Gabriel Jesus akitumbukiza goli la pili la Manchester City
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni