Tottenham Hotspur wameonyesha
kiwango cha juu cha kuhimili mikiki mikiki ya Real Madrid na
kufanikiwa kutoka sare ya goli 1-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa
Ulaya.
Katika mchezo huo Tottenham Hotspur
ilikuwa ya kwanza kupata goli baada ya Kane kumkimbilia beki Raphael
Varane na kumlazimisha kutumbukiza katika goli lake mpira wa krosi.
Goli hilo la dakika ya 28, lilidumu
hadi katika dakika ya 43 pale Cristiano Ronaldo alipofunga goli kwa
mkwaju wa penati.
Mpira uliopigwa na beki Raphael
Varane kwa nia ya kuuokoa ukijaa wavuni na kujifunga
Mshambuliaji nyota duniani Cristiano Ronaldo akifunga goli la kusawazisha kwa mkwaju wa penati
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni