Nyota wa filamu wa Hollywood Mkenya
Lupita Nyong'o amekuwa miongoni mwa wanawake waliojitokeza hadharani
kumtuhumu bilionea Mtayarishaji filamu Harvey Weinstein kwa kumtaka
kimapenzi ili amsaidie kumtoa katika filamu.
Lupita mshindi wa tuzo ya Oscar kwa
uhusika wake kwenye filamu ya '12 Years a Slave', ameeleza kuwa
bilionea huyo alijaribu kumshawishi kufanya naye mapenzi wakati akiwa
mwanafunzi muigizaji katika shule ya Uigizaji ya Yale.
Lupita amesema alikutana na
Weinstein mwaka 2011 katika tamasha la filamu na kumualika nyumbani
kwake kwenda kuangalia filamu mpya aliyoitayarisha, ambapo alikubali
na kwenda kuangalia.
Amesema wakiwa nyumbani waliangalia
filamu hiyo na watoto wake, kisha akamuita Lupita akampeleka katika
chumba na kumuambia anataka kumfanyia masaji, jambo ambalo Lupita
alidhani kuwa ni mzaha.
Lupita katika kujaribu kujiokoa
akamtaka Mtayarishaji huyo ndiyo alale chini ili amfanyie masaji ili
iwe rahisi kumdhibiti iwapo atataka kumbaka kuliko yeye kulala chini
na Weinstein kumfanyia masaji jambo ambalo lingemuhatarisha.
Wakati Lupita akimfanyia masaji
Weinstein, alitaka kuvua suruali yake ili amfanyie masaji sehemu ya
chini ya kiuno, ndipo Lupita alipogoma na kumuambia hatojisikia
vizuri na baada ya hapo waliagana na kuondoka.
Mtayarishaji filamu bilionea Harvey Weinstein anakabiliwa na tuhuma za kuwadhalilisha kingono waigizaji filamu wakike kadhaa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni