Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger,
amesema timu yake imeonyesha uwezo kwa kuendelea kufanya vizuri Ligi
ya Uropa baada ya kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Crvena Zvezda
huko Serbia.
Shujaa wa mechi hiyo alikuwa
mshambulia Olivier Giroud aliyefunga goli kwa tik-taka katika dakika
za mwisho dhidi ya Crvena Zvezda iliyobakia na wachezaji 10, na
kuifanya kushinda mechi tatu katika kundi lao la H.
Olivier Giroud akiwa ameanguka chini baada ya kuupiga mpira uliozaa goli kwa staili ya tik-taka
Mchezaji wa Crvena Zvezda Milan Rodic akipewa kadi nyekundu ndani ya dakika 10 tu za mchezo huo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni