Na Mwandishi wetu,
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imefanya mazungumzo na Taasisi mbili muhimu za kifedha na kiuchumi nchini China kwa ajili ya upatikanaji wa fedha za uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu na viwanda nchini Tanzania hususan kwenye Sekta ya Kilimo.
Majadiliano hayo yalifanywa kati ya Ujumbe wa TADB ulioongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki , Bw. Francis Assenga alipokutana na Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya China (CBD) kwenye Mkutano uliofanyika Shangrila Hotel, Guangzhou China wakati wa Kongamano la Pamoja la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na China.
Pande zote mbili zilikubaliana kuendelea na kuimarisha ushirikiano utakaowezesha kupatikana kwa fedha kwenye uwekezaji wa miundo mbinu ya kilimo na viwanda vidogo vidogo vya uongezaji thamani kwenye mazao ya kilimo kwa wakulima nchini.
Katika ziara hiyo TADB pia ilifanya majadiliano ya kina na Mfuko wa Maendeleo ya Africa wa China (China African Development Fund) ambao hufanya uwekezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo na ya kibiashara (Equity investmenta) kwenye nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.
Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na Ujumbe wa ulioongozwa na Makamu Mtendaji wa Rais na Naibu Mtendaji Mkuu wa 'CADFUND' Bwn. Wang Yong aliyefuatana na Mkurugenzi Mkuu wa Sekta ya Viwanda, Kilimo, Afya na Uwekezaji, Bw. Lei Ma; Mkurugenzi Mkuu wa Maendeleo ya Masoko na Huduma Elekezi Bw. Henry Liu; na Meneja wa Uwekezaji wa Viwanda, Ardhi na Kilimo Bw. Luo Zhongquan.
Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji (UWEKEZAJI), Prof. Adolf Mkenda. Wengine waliohudhuria ni Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki; na Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini China Bw. Lusekelo Gwassa.
Katika mazungimzo hayo, pamoja na mambo mengine CADFUND walikubali kuendelea kutoa fedha kwenye miradi ya kiuchumi na uwekezaji mkubwa kwenye nyanja kuu nne zikiwemo kilimo; viwanda; madini; na miundombinu kama ya maji na umwagiliaji.
Aidha CADFUND na TADB ziliainisha maeneo kadhaa ya ushirikiano kama vile Uhakiki na Usimamizi wa miradi; Utafiti; Ukaguzi; na Ujengaji wa Uwezo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni