Shule ya Sekondari ya Lokichogio AIC
iliyopo Turkana nchini Kenya imeshambuliwa na majambazi ambao
inasemekana wanatokea Sudani Kusini.
Katika tukio hilo linalodaiwa
kumshirikisha mwanafunzi mmoja aliyesimamishwa masomo, jumla ya
wanafunzi watano wameuwawa pamoja na mlinzi mmoja.
Majeruhi walionamajeraha madogo
wametibiwa katika hospitali ya Lopiding iliyopo Lokichiogio na
waliojeruhiwa vibaya wamepelekwa hospitali ya rufaa ya Lodwar.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni