Mabingwa watetezi wa kombe la
Carabao Manchester United wametinga robo fainali ya michuano hiyo
kiulaini kwa kupata ushindi mwepesi wa magoli 2-0 dhidi ya Swansea
City.
Kikosi cha Manchester United
kilichofanyiwa mabadiliko makubwa kiliutawala mchezo huo na kupata
goli la kwanza kupitia kwa Jesse Lingard kufuatia pande la kisigino
la Marcus Rashford.
Wageni Manchester United waliongeza
goli la pili kwa shambulizi zuri ambapo mpira ulimkuta Lingard na
kufunga kwa mpira wa kichwa.
Jesse Lingard akipiga mpira uliozaa goli la kwanza la Manchester United
Mshambuliaji Marcus Rashford akiwatoka wachezaji wa Swansea
City
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni