Kipa Claudio Bravo ameibuka kuwa
shujaa wa Manchester City katika mchezo wa jana dhidi ya Wolves
baada ya kupangua mikwaju ya penati na kutinga robo fainali ya kombe
la Carabao.
Bravo, aliyeokoa michomo mitatu
katika muda wa kawaida aliongeza kuonyesha ushujaa wake kwa kupangua penati za Alfred
N'Diaye na Conor Coady baada ya mchezo kuisha kwa sare tasa.
Manchester City ilifunga penati zote
nne huku, Sergio Aguero kumalizia kiufundi penati ya nne na kufanya
matokeo kuwa 4-1.
Kipa wa Manchester City Claudio Bravo akipangua penati ya Alfred
N'Diaye
Sergio Aguero akishangilia baada ya kutumbukiza golini mpira wa penati
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni