Miujiza ya Lionel Messi imeisaidia
Argentina kukata tiketi ya fainali za kombe la dunia Urusi 2018,
baada ya nyota huyo wa Barcelona kuifungia timu yake ya taifa
hat-trick.
Argentina ilifanikiwa kujihakikishia
nafasi hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya
Ecuador huko Quito jana.
Romario Ibarra aliipatia Ecuador
goli la kuongoza kabla ya Lionel Messi kusawazisha kufuatia kugongena
vyema na Angel Di Maria.
Messi tena akafunga goli la pili kwa
shuti la mguu wake wa kushoto na kisha akakamilisha hat-trick yake ya
44 katika maisha yake ya soka baada ya dakika ya 62.
Lionel Messi akishangilia kwa kubeba mpira baada ya kufunga goli la kwanza
Lionel Messi akitumbukiza goli la pili huku akiwaacha hoi mabeki wa Ecuador



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni