Akizungumza kwenye maadhimisho ya 72 ya Umoja wa Mataifa (UN) na wageni waalikwa kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassani amesema kwamba maendeleo ya viwanda yanakwenda sambamba na tishio la uharibifu wa mazingira na tabianchini ni muhimu kwa wadau wote wa maendeleo kujipanga.
“Sote tunajua kwamba maendeleo ya viwanda yalikuja na uharibifu mkubwa wa mazingira na hali ya hewa katika kipindi cha mapinduzi ya viwanda kipindi kile cha karne ya 18th na 19th sasa ni muhimu kwa mataifa yaliyopiga hatua za kisayansi na teknolojia kuweza kuwa tayari kusaidia kwenye hili,” amesema Makamu wa Rais.
Amesema nchini juhudi zinaendelea za kukuza uchumi na maendeleo ya watu lakini ni muhimu kwa wananchi kwa ujumla wao kuweza kulinda na kuhifadhi zaidi maliasili, hifadhi na rasilimali za taifa ili kuweza kufikia uchumi wa viwanda.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni