Kongamano hilo kubwa lenye uhamasishaji mkubwa wa uwekezaji wa Viwanda nchini Tanzania,limeandaliwa na Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies na litawashirikisha wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda na makampuni wapatao zaidi ya 200 kutoka majimbo mbalimbali nchini China.
Balozi Kairuki amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies Mohamed Kiluwa kwa kuonesha juhudi kubwa za kuwahamasisha na kutafuta washirika mbalimbali katika suala zima la uwekezaji wa viwanda nchini Tanzania.
Balozi Kairuki amesema kuwa,Kampuni ya Kiluwa kwa kufanya hivyo wanaibeba dhana ya Tanzania ya Viwanda kwa
utekelezaji kwa vitendo,na pia kuunga mkono dhamira ya Rais Dkt John Pombe
Magufuli ya kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya Viwanda,na kuongeza kuwa yuko tayari kutoa kutoa ushirikiano wa kutoka katika suala zima la kuwahamasisha wawekezaji kutoka nchini China na kwenda kuwekeza nchini tanzania katika suala zima la Viwanda.
Mkurugezi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Naima Kiluwa akiandika kilichokuwa kikijiri kwenye mazungumzo hayo mafupi na Balozi Mh.Mbelwa Kairuki mara baada ya kuukaribisha ujumbe huo Ubalozini kwake na kuzungumza mambo mbalimbali yaliyohusu masuala ya uwekezaji kwa Tanzania,na baadae kupata chakula cha pamoja.
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa kairuki akimkabidhi zawadi mmoja wa watakaoshiriki Kongamano la Viwanda linalotarajia kufanyika kesho mjini Beijing,likatalojumuisha Wamiliki wa Viwanda,Wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali wapatao zaidi ya 200,anaeshuhudia kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa Pwani, Zuberi Semataba
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa kairuki akimkabidhi zawadi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Mohamed Said Kiluwa
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe.Mbelwa kairuki akimkabidhi zawadi Mkurugezi Mtendaji wa Kampuni ya Kiluwa Industrial Group of Companies,Naima Kiluwa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni