Wakati timu zilizofuzu kutinga
fainali za kombe la dunia zikijulikana, michuano hiyo itawakosa nyota
kadhaa ambao timu zao za taifa hazijafanikiwa kupata tiketi ya
michuano hiyo.
Miongoni mwa wachezaji hao ni Arjen
Robben, wa Uholanzi na timu ya Bayern Munich, kiungo Christian
Pulisic, wa Marekani na klabu ya Borussia Dortmund.
Wengine ni kiungo Arturo Vidal wa
Chile na timu ya Bayern Munich, kiungo Naby Keita, wa Guinea na klabu
ya RB Leipzig pamoja na Gareth Bale wa Wales timu ya Real Madrid.
Pia wamo Pierre-Emerick Aubameyang
wa Gabon na klabu ya Borussia Dortmund, Alexis Sanchez wa Chile na
timu ya Arsenal, Antonio Valencia wa Ecuador na Manchester United.
Mshambuliaji Gareth Bale hatashiriki fainali za kombe la dunia
Arturo Vidal wa Chile naye hataonekana Urusi kwenye kombe la dunia
Pierre-Emerick Aubameyang
wa Gabon naye hatokuwepo Urusi 2018




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni