.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 27 Oktoba 2017

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Oktoba 26, 2017 amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wakiwemo Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wa Wizara, Mabalozi pamoja na Wakuu wa Mikoa.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akisoma majina ya walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam leo Oktoba 26, 2017

Uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu wao

Ofisi ya Rais Ikulu - Katibu Mkuu Alifayo Kidata

Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na utawala Bora - Katibu Mkuu Dr. Lawrian Ndumbaro

Naibu Katibu Mkuu - Bi. Dorothy Mwaluko

Ofisi ya Rais TAMISEMI - Katibu Mkuu Eng. Mussa Iyombe

Naibu Katibu Mkuu (TAMISEMI Afya) - Zainabu Chaula

Naibu Katibu Mkuu (TAMISEMI Elimu) - Dickson Nzunda

Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira - Katibu Mkuu Eng. Joseph Kizito Manongo (alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo hiyo)

Naibu Katibu Mkuu - Bi. Butamo Kasuka Philipo

Ofisi ya Waziri Mkuu

Kazi na Ajira - Katibu Mkuu Erick Shitindi

Bunge na Waziri Mkuu - Katibu Mkuu Bi. Maimuna Tarishi

Sera - Katibu Mkuu Faustine Kamuzora (amehamishwa kutoka ofisi ya makamu wa rais)

Wizara ya Kilimo - Katibu Mkuu Eng. Mathew Mtigumwe

Naibu Katibu MKuu - Dr. Tomas Didim Kashilila

Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Mifugo - Katibu Mkuu Dr. Maria Mashingo

Uvuvi - Katibu Mkuu Dr. Yohana Budeba

Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano

Uchukuzi - Katibu Mkuu Dr. Leonard Chamuriho

Ujenzi - Katibu Mkuu Eng. Joseph Nyamuhanga

Mawasiliano - Katibu Mkuu Dr. Maria Msasabo

Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano - Eng. Adelina Madete

Wizara ya Fedha na Mipango - Katibu Mkuu Dotto James Mgosha

Naibu Katibu Mkuu Utawala - Bi. Suzan Mkapa

Naibu Katibu Mkuu Fedha za Nje - Bi. Amina Shaaban

Naibu Katibu Mkuu Sera - Dr. Hakingu M. Kazungu

Wizara ya Nishati - Katibu Mkuu Dr. Hamis Mwinyimvua (Anatoka ofisi ya Waziri Mkuu)

Wizara ya Madini - Katibu Mkuu Prof. Saimon S. Msanjila (alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu)

Wizara ya Katiba na Sheria - Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome > Naibu Katibu Mkuu - Bwana Amon Mbanju

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - Katibu Mkuu Prof. Adolph Mkenda (ambaye ni Mchumi, anatoka Wizara ya Biashara na Uwekezaji).

Naibu Katibu Mkuu - Balozi Ramadhan Muomba Mwinyi

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Katibu Mkuu Dr. Florence Nduruka

Naibu Katibu Mkuu - Bi. Emmaculate Peter Ngwale

Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa

Mkoa wa Manyara - Mkuu wa Mkoa ni Alexandar Pastor Mnyeti (Alikuwa DC wa Arumeru)

Mkoa wa Rukwa - Mkuu wa Mkoa ni Joachim Leonard Wangabo (alikuwa DC wa Nanyumbu)

Mkoa wa Geita - Mkuu wa Mkoa ni Bwana Robert Gabriel Lughumbi (alikuwa DC wa Korogwe)

Mkoa wa Mara - Mkuu wa Mkoa ni Adam Kigoba Ally Malima (aliwahi kuwa kwenye baraza la mawaziri awamu ya nne)

Mkoa wa Dodoma - Mkuu wa mkoa ni Bi. Christine Solomoni Mndeme (alikuwa DC wa Dodoma Mjini)

Mkuu wa Mtwara - Gelasius Gasper Byakanwa (alikuwa DC wa Hai)

Uteuzi wa Mabalozi

Dr. Aziz P. Mlima - Ameteuliwa kuwa Balozi (alikuwa Katibu Mkuu wizara mambo ya nje)

IGP Mtaafu Ernest Mangu - Ameteuliwa kuwa Balozi

Hawa Vituo vyao vya kazi vitatangazwa.

Wote wanatarajiwa kuapishwa kesho saa nane mchana.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni