iliyoambatana na upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira katika shule ya
sekondari ya Mukulat iliyopo Mkoani Arusha shughuli iliyohudhuriwa na
wafanyakazi wa shirika hilo ,wazazi na wadau wa elimu jana (Habari Picha Na Pamela Mollel,Arusha)
Afisa Elimu Taaluma Halmashauri ya Wilaya Arusha Vijijini ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri akimkabidhi zawadi iliyotolewa na bodi ya shule kwa Mkurugenzi wa Haki Elimu nchini John Kalage kwa kutambua umuhimu wa elimu Nchini
Shirika lisilo la kiserikali nchini Haki Elimu limetoa shilingi milioni ishirini ya kuanzishwa kwa ujenzi wa kisima cha maji katika shule ya sekondari mukulat katika kijiji cha lemanyata kata ya lemanyata wilaya ya arusha vijijini ili kuwaondolea adha wanafunzi i wa shule hiyo wanaolazimika kusafiri umbali mrefu na kutumia muda mwingi kwakutafuta maji.
Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na uapandaji wa miti na utunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya Mukulat Mkurugenzi wa haki elimu nchini john kalaghe amesema shirika la haki elimu limeamua kushirikiana na jamii katika kuondoa changamoto katka sekta ya elimu katika shule hiyo ikiwamo tatitzo la maji pamoja na kuboresha mazingira kwa kupanda miti pamoja na kukarabati majedarasa hayo kwa kupiga rangi.
Shirika hilo la haki elimu kwa kupitia kwa mkurugenzi huyo wameahidi kutoa ufadhi kwa kuwalipia karo wanafunzi wa shule ya sekondani ya mukulat watakaofanya vizuri kwa ufaulu wa daraja la kwanza katika mtihani wa kidato cha nne unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni ili kutoa hamasa kwa wanafunzi wengine kufanya vizuri katika mitihni hasa kwa mtoto wa kike ambaye anaonekana yuko nyuma kwa mambo ya elimu hasa katika jamii ya
kifugaji.
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaa ya Arusha vijijini katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii ,afisa elimu wa wilaya hiyo B akari kimath amelipongeza shirika la haki elimu kwa kuanzisha mradi wa maji katika shule hiyo pamoja na upandaji wa miti na ukarabati wa madarasa na amesema miradi hiyo itapunguza changamoto za elimu zinazozikabili shule za msingi na sekndari wilayani humo na kuliomba shirika hilo kuendela na msaada huo katika shule zilizoko pembezoni mwa wilaya ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora
Ameiomba jamii kushirikiana na mashirika yasyoyakiserikali kupungumza changamoto yanaozikabili shule za msingi na sekondari na kuitaka jamii kuhakikisha wanatunza miradi hiyo ili iweze kuwasaidia wanafunzi
walikuwa wanapata shida kwa usafuri umbali mrefu kutafuta maji.
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha miradi shirika la haki elimu Boniventura Godfrey amesema kwa kutambua changamoto zinazoikabili
sekta ya elimu nchni tayari wameanzisha mpango maalumu wa kuzisaidia shule za msingi na sekondari 127 katika wilaya ishirini na mbili kwa kuwasaidia miradi ya maji,uwekaji wa umeme wa jua ,ukarabati wa madarsa,na upelekaji wa vifaa vya elimu ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu katika mzngira bora.
Awali wakizungumzi miradi hiyo wanafunzi wa shule ya sekondari Mukulat Stella Massawe wamelishukuru shirika la haki elimu kwa uboreshaji wa miundombinu katika shule hiyo kwa kuwa mradi huo wa maji utawapungumzia changamoto iliyokuwa ikiwakabili kwa kusafuri umbali mrefu kwa kutafuta maji pamoj na kutumia muda wa masomo hivyo ,kupungua kwa changamoto hizo kutapunguza suala la utoro kwa wanafunzi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni