Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na
Neymar wametajwa katika kikosi bora cha wachezaji 11 wa Shirikisho la
Soka la Fifa.
Ronaldo ameungana katika orodha hiyo
na nyota wenzake wa Real Madrid ambao ni Marcelo, Sergio Ramos, Luka Modric
pamoja na Toni Kroos.
Kipa Gianluigi Buffon, aliyetwaa
tuzo ya kipa bora wa Fifa naye yumo katika kikosi hicho, huku Dani
Alves, Andres Iniesta na Leonardo Bonucci wakikamilisha kikosi hicho.
Wachezaji wa kikosi Bora cha Wachezaji 11 wa Fifa wakipiga picha na mshereheshaji Idris Elba ambaye ni muigizaji nyota wa filamu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni