Crystal Palace imepata ushindi wa
kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kufungwa mechi saba
mfululizo baada ya kuibuka nyumbani na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya
Chelsea.
Katika mchezo huo Chelsea walijikuta
wakifungwa goli la kwanza kupitia jitihada za Yohan Cabaye, lakini
goli hilo lilisawazishwa baadaye na Tiemoue Bakayoko.
Wilfred Zaha aliyerejea dimbani
baada ya kupona kufuatia kuwa majeruhi kwa muda ndiye aliyelizamisha
jahazi la mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Wachezaji wa Chelsea wakishangilia baada ya Tiemoue Bakayoko kufunga goli
Mshambuliaji Wilfred Zaha akifunga goli la pili la Crystal Palace na kuizamisha Chelsea
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni