.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 11 Novemba 2017

ITALIA HATARINI KUZIKOSA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA

Kocha wa Italia Giampiero Ventura amesema kuwa kikosi chake kitahitaji kuongeza kiwango chake katika mchezo wa marudio na Sweden ili kuepuka kukosa michuano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu 1958.

Timu ya taifa ya Sweden imeshinda mchezo wa kwanza kwa goli 1-0 katika dimba la Friends Arena, goli hilo pekee likifungwa na Jakob Johansson akiachia shuti la umbali wa yadi 20 kufuatia krosi ya Daniele de Rossi iliyogongwa.

Italia ilionekana kuimarika katika kipindi cha pili cha mchezo huo lakini kiwango hicho walichoonyesha hakikuisaidia kusawazisha goli hilo, licha ya Matteo Darmian kukaribia kufunga lakini shuti lake likagonga mwamba.
       Mpira uliopigwa na Jakob Johansson ukiwa umetinga wavuni mwa lango la Italia

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni