.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 14 Novemba 2017

ITALIA KUIKOSA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA YA MWAKA 2018 URUSI

Mabingwa mara nne wa kombe la dunia Italia wameshindwa kufuzu fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958 baada ya kushindwa kuifunga Sweden katika mchezo wa marudio.

Hii inaamaana Italia maarufu kama Azzurri hawatokuwepo katika michuano hiyo ya soko ya dunia nchini Urusi mwakani, ikiwa ni mara ya pili kujikuta kuwa katika hali hiyo katika historia ya michuano hiyo tangu mwaka 1930.

Goli la kiungo Jakob Johansson la shuti lililogongwa na kumpoteza mahesabu kipa katika mchezo wa kwanza lilitosha kuifungasha virago Italia baada ya jana kutoka sare tasa huko Milan katika dimba la San Siro.
        Wachezaji wa Sweden wakishangilia kufanikiwa kufuzu fainali za kombe la dunia
Kipa wa Italia Gianluigi Buffon akipungia mashabiki kwa huzuni kuwaaga baada ya kutangaza kustaafu soka la kimataifa

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni