.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 15 Novemba 2017

KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU, DK. AKWILAPO AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA ELIMI

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo amefungua mkutano wa 9 kwa wadau wa sekta ya elimu nchini ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT) ukiwa na lengo la kuangalia ubora na usawa wa elimu maeneo yote.

Warsha hiyo ya siku tatu ambayo imeanza leo mjini Dodoma na kukutanisha mashirika mbalimbali wadau wa elimu kujadili namna ya kuboresha ufudishaji na ujifunzaji kwenye sekta ya elimu pamoja na kuimarisha hali ya utoaji elimu kwa ujumla.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Dk. Leonard Akwilapo alisema baada ya mafanikio ya awali katika kuongeza udahili wa wanafunzi katika ngazi zote za elimu, yaani kuanzia ngazi ya awali, elimu ya msingi, elimu ya sekondari na elimu ya juu nafasi iliyobaki ni kuboresha elimu yenyewe kwa ujumla.

Alisema eneo hilo Serikali itahakikisha wanafunzi wanaohitimu wanapata stadi mbalimbali ambazo zimepangwa kulingana na mtaala katika ngazi hiyo. Aliwataka washiriki wa warsha hiyo kuangalia matatizo na fursa anuai zilizopo kwenye sekta ya elimu, pamoja na njia mbalimbali za kuweza kuboresha kisha mapendekezo hayo yawasiliswe Serikalimi ili kuangalia namna ya kufanyiwa kazi.

Alisema katika mfumo wa sasa Serikali inatambua kuwa zipo baadhi ya shule zinazotoa elimu katika mazingira ambayo sio mazuri, lakini lengo lililopo ni kuhakikisha wanafanya maboresho ili kuondoa changamoto hizo.

"..Tunatambua kwamba katika mfumo wetu wa elimu bado tuna shule ambazo zina hali ambayo sio nzuri, lengo la Serikali ni kuhakikisha zile shule zote ambazo zina hali mbaya sana zinaboreshwa...mfano zile ambazo zina mapaa ya nyasi tunataka zote tuzitoe ili kuongeza hamasa ya walimu na wanafunzi katika kupata elimu, Serikali kwa sasa tumesha sambaza vifaa kama vya maabara, vitabu na yote ni kuhakikisha tunaboresha," alisema Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Kwa upande wake Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Cathleen Sekwao ambao ni waandaaji wa mkutano huo, alisema sera ya elimu bila ada imekuwa ni nzuri licha ya uwepo wa changamoto mbalimbali ikiwemo ongezeko kubwa la wanafunzi kuanzia mwaka jana. Alizitaja changamoto hizo ni pamoja na upungufu wa vyumba vya madarasa, upungufu wa walimu na miundombinu ya elimu vikiwemo vitendea kazi.

Bi. Sekwao alisema Serikali imejitahidi kuhamasisha wananchi kujiunga kusaidiana kukabiliana na changamoto mbalimbali na wao kama asasi za kiraia zinazo tetea elimu bora yenye usawa wamesaidia pia katika ujenzi wa madarasa, uchangiaji wa vifaa na kuhamasisa wananchi kusaidia utatuaji changamoto hiyo.

Aidha aliongeza kuwa na wao asasi zisizo za serikali wameungana kuisaidia Serikali ambapo zipo asasi zilizojenga madarasa, zimejenga nyumba za walimu na zingine kuhamasisha wananchi kuchangia maboresho ya elimu hali ambayo imeanza keleta chachu maeneo mbalimbali nchini.

Alisema lengo la mkutano huo ni kuangalia usawa wa elimu katika maeneo yote yaani vijijini na mijini ikiwemo kujadiliana na kushauri maboresho yenye tija katika sekta ya elimu kulingana na mahitaji ya sasa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo akifungua mkutano wa 9 kwa wadau wa sekta ya elimu nchini ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT). Mkutano huo umeanza leo New Dodoma Hoteli, Mkoani Dodoma.
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Cathleen Sekwao akizungumza leo kwenye mkutano wa 9 wa wadau wa sekta ya elimu nchini ulioandaliwa na TenMeT. Mkutano huo wa siku tatu umeanza leo New Dodoma Hoteli, Mkoani Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa huo uliokutanisha mashirika mbalimbali wadau wa elimu kujadili namna ya kuboresha ufudishaji na ujifunzaji kwenye sekta ya elimu pamoja na kuimarisha hali ya utoaji elimu kwa ujumla wakifuatilia mada mbalimbali.
Sehemu ya washiriki wa huo uliokutanisha mashirika mbalimbali wadau wa elimu kujadili namna ya kuboresha ufudishaji na ujifunzaji kwenye sekta ya elimu pamoja na kuimarisha hali ya utoaji elimu kwa ujumla wakifuatilia mada mbalimbali.
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Cathleen Sekwao (kulia) akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo mara baada ya kufungua mkutano wa 9 kwa wadau wa sekta ya elimu nchini ulioandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT).
Dk. Mkonongwa akiwasilisha mada kwenye mkutano huo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni