.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 13 Novemba 2017

SHIRIKA LA AMREF LAZINDUA MRADI WA UCHECHEMUZI KATIKA SEKTA YA AFYA MKOANI SHINYANGA

 Mgeni rasmi, Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dkt.Rashid Mfaume akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi huo huku viongozi mbalimbali wakishuhudia.

Shirika la Amref Health Africa hii leo limezindua mradi wa uchechemuzi katika sekta ya afya (Health System Advocacy HSA) mkoani Shinyanga, wenye lengo la kuongeza ushawishi katika sekta ya afya ili kuboresha zaidi sekta hiyo mkoani humo.

Meneja mradi huo, Josiah Otege amesema lengo ni kufanya uchechemuzi (ushawishi) katika maeneo manne ya sekta ya afya ambayo ni kuimarisha uzazi wa upango, bajeti ya afya, kuongeza idadi ya watumishi wa afya, kuboresha afya ya uzazi pamoja na utawala bora katika sekta hiyo.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, mgeni rasmi Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Dkt.Rashid Mfaume ambaye alimwakilisha Katibu Tawala mkoani humo Albert Msovela, alilipongeza shirika la Amref kwa kuanzisha mradi huo ambao alisema utasimamiwa vyema ili kuhakikisha unaleta mabadiliko chanya katika jamii.

Mradi huo ambao ni wa miaka minne kuanzia mwaka huu, unatarajiwa kutekelezwa katika halmashauri tatu za mkoa wa shinyanga ambazo ni Msalala, Shinyanga Vijijini pamoja na Kishapu.

                   Meneja mradi huo wa HSA, Josiah Otege akizungumzia mradi huo.
                                                                                             Na Binagi Media Group

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni