Taasisi ya Kifedha inayoongozwa na
mfanyabiashara mwanamke Muingereza Amanda Staveley imewasilisha dau
la paundi milioni 300 kuinunua klabu ya Newcastle United.
Kampuni hiyo ya PCP Capital Partners
imefanya mazungumzo na mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley kwa mwezi
sasa, na taarifa sasa zinasema dau hilo limetengwa.
Uongozi wa klabu ya Newcastle
haujazungumzia lolote kuhusiana na ofa hiyo, ingawa chanzo kimoja
ndani ya klabu hiyo hakijaridhika na kiasi cha dau hilo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni