Chama cha rais wa Zimbabwe Robert
Mugabe ambaye yupo matatani kwa sasa kimeanza mchakato wa kumchukulia
hatua.
Afisa mmoja wa Zanu-PF amesema hoja
ya kumvua madaraka ya urais Mugabe itawasilishwa bungeni hii leo, na
mchakato huo utachukua siku mbili tu.
Hoja hiyo inamtumuhu Mugabe 93
makosa kadhaa likiwemo la kumruhusu mkewe Grace kujitwalia madaraka
ya Kikatiba.
Viongozi wa kijeshi waliodhibiti
nchi hiyo wiki iliyopita wamesema hivi karibuni watakutana na
aliyekuwa makamu wa rais aliyekimbia uhamishoni baada ya kutimuliwa.
Wananchi wa Zimbabwe wakiandamana mitaani kushinikiza rais Robert Mugabe ajiuzulu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni