.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 3 Novemba 2017

TIMU YA EVERTON YATOLEWA NJE LIGI YA UROPA NA LYON

Everton waliobakia 10 uwanjani wametolewa nje ya Ligi ya Uropa baada ya kuchapa magoli 3-0 na Lyon, na kutibua matumaini ya David Unsworth kuteuliwa kuwa kocha wa kudumu wa timu hiyo.

Mchezaji wa zamani wa Chelsea Bertrand Traore alianza kutikisa nyavu katika dakika ya 68 baada ya kuwazidi kasi mabeki wa Everton na kutumbukiza mpira uliomshinda kipa Jordan Pickford.

Mambo yalizidi kuwa magumu pale Morgan Schneiderlin alipopewa kadi ya pili ya njano kwa kumchezea rafu Maxwel Cornet.

Mchezaji wa zamani wa Manchester United Memphis Depay alimpa pande Houssem Aouar na kufunga la pilina kisha baadaye Depay akakamilisha karamu kwa kufunga goli la tatu.
                  Morgan Schneiderlin akitoka nje baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu
                             Mchezaji wa zamani wa Chelsea Bertrand Traore akifunga goli

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni