.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 2 Novemba 2017

TIMU YA TOTTENHAM YAIFANYIA KITU MBAYA REAL MADRID

Timu ya Tottenham imefuzu kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kutandaza soka safi na kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Real Madrid katika dimba la
Wembley.

Spurs, ikicheza ikiwa na nyota wake mshambuliaji Harry Kane ambaye amerejea uwanjani baada ya kupona maumivu ya paja, ilionyesha kiwango kizuri cha soka na alikuwa Dele Alli aliyefunga goli la kwanza katika dakika ya 27.

Dele Alli tena akaifungia Tottenham goli la pili katika kipindi cha pili kisha Christian Eriksen akafunga goli la tatu akiunganisha kwa utulivu krosi ya Kane, kabla ya Cristiano Ronaldo kufunga goli pekee la Real Madrid.
                                    Mshambuliaji Dele Alli akifunga goli la kwanza la Tottenham
          Cristiano Ronaldo akiwa ameshika kiuona baada ya jahazi ya Real Madrid kuzama

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni