.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 7 Desemba 2017

ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA MANYARA JOEL BENDERA AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera ( pichani ) amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Marehemu Joel Nkaya Bendera alipokelewa katika hospitali ya Taifa Muhimbili saa 6:03 mchana na kupelekwa kwenye huduma ya matibabu ya dharula, lakini ilipofika saa 10:24 jioni aliaga Dunia.

Bendera amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo. 

Pia wanamichezo watamkumbuka sana Joel Bendera kama kocha wa Taifa Stars iliyoshiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 1980 nchini Nigeria.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni