Watu wapatao 36 wamekufa katika
ajali ya barabarani baada ya basi lililojaa abiria likielekea Nairobi
kugongana na lori katika eneo la Migaa katika barabara kuu ya
Nakuru-Eldoret.
Miongoni mwa waliokufa ni pamoja na
dereva wa lori pamoja na utingo wake ambao lori lao lilikuwa
linaelekea Eldoret, ambapo miili 28 ya watu waliokufa papo hapo
imetolewa kwenye eneo la ajali hiyo mbaya.
Watu 30 wameripotiwa kufa papo hapo
na wengine wanne walifariki duniani baadaye wakipatiwa matibabu ya
majeraha yao kwenye hospitali ya Nakuru Level Five.
Miongoni mwa wanne waliokufa
hospitali ni watoto watatu wenye umri wa miezi miwili, mtoto wa miaka
miwili mmoja na wa miaka 10 mmoja pamoja na mtu mzima mwenye umri wa
miaka 35.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni